OSHA : KUMEKUWA NA ONGEZEKO WAFANYAKAZI KUPATA MAFUNZO USALAMA MAHALI PA KAZI.

📌RHODA SIMBA

WAKALA wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), umesema kumekuwa na ongezeko la wafanyakazi waliopata mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kutoka wafanyakazi 32,670 hadi kufikia wafanyakazi 43,318, ambapo ni sawa na asilimia 175.

Mafunzo hayo yanajumuisha mafunzo ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na uundwaji wa kamati za Usalama na Afya.

Hayo yamesemwa leo Machi 4 2023,  jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Khadija Mwenda wakati akizungumza na waandishi wa habari Katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuelezea utekelezaji wa majukumu ya  Wakala huo na vipaumbele vyake.

 

Post a Comment

0 Comments